KUMBUKIZI YA WAASISI WA GIRL GUIDES (WIKI YA HUDUMA)

Kumbukizi ya Waasisi wa Girl Guides duniani, ijulikanayo kama, “World Thinking Day” huadhimishwa tarehe 22 Februari kila mwaka na Girl Guides wote ulimwenguni. Ni siku ambayo Girl Guides hutumia kuwafikiria Girl Guides wenzao kutoka mataifa yote duniani, na kuangazia maswala mazima ya Guiding na umuhimu wake kimataifa.

Hivi karibuni, Chama cha Maskauti wa kike duniani (WAGGGS) kilichagua maswala mtambuka ya kimataifa kama kaulimbiu ya maadhimisho ya kumbukizi ya Waasisi wa Girl Guides ulimwenguni. Girl Guides hutumia nafasi hiyo kujifunza na kuheshimu tamaduni za nchi zingine,  usawa na  kuongeza uelewa juu ya maswali mbalimbali kimataifa.

Wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, Girl Guides wa chini ya umri wa miaka 18 kutoka nchi 100, waliulizwa ni maswala gani ambayo wanatamani yaangaliwe kwa jicho la pili na wangependa kubadilisha katika ulimwengu wa sasa. Kwa kupitia ukusanyaji wa taarifa hizo ikaonekana kuwa wengi wao walikua na wasiwasi na swala zima la mazingira. Hivyo basi Kaulimbiu za Siku hiyo kwa mwaka 2022 – 2024  zitakua, “Dunia Yetu, Mustakabali wetu” ambapo kila mwaka Girl Guides watakua wanaangazia Mustakabali ambao wanatamani kuishi

Kwa mwaka huu 2023, Kaulimbiu Ya “Dunia Yetu, Mustakabali Wetu” imeangazia kwenye maswala mazima ya Mazingira na Amani, ambapo kupitia mtaala wa World Thinking Day 2023, wasichana wamepata nafasi ya kuangalia ni kitu gani wanaweza kujifunza kwenye mazingira na namna gani wanaweza kufanya kazi na uoto wa asili ili kutengeneza kesho yenye amani na ulinzi kwa kila msichana duniani.

Wiki moja kabla ya Maadhimisho ya kumbukizi ya waasisi wa Girl Guides duniani, Girl Guides hupaswa kushiriki katika Wiki ya Huduma (Service Week), ambapo kwa mwaka huu, Girl Guides kutoka mikoa 12 ya ki Girl Guides (Arusha, Bagamoyo, Kisarawe, Shinyanga, Ruvuma, Temeke, Kinondoni, Tanga, Lindi, Singida, Tabora, na Kigamboni) walipata nafasi ya kuandaa na kushiriki katika matukio mbali mbali ikiwemo, Kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa mahospitalini, kutembelea watoto yatima na wenye mahitaji maalumu, lakini pia waliweza kushiriki katika kufanya usafi na utunzaji wa Mazingira uliohusisha moja kwa moja upandaji wa miti, na usafi wa maeneo ya shule na mazingira yanayowazunguka.

MATUKIO YA PICHA

Girl Guides Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, walifanikiwa kupanda miche 3500 ya miti ya mikoko wilayani humo

Post a comment

Your email address will not be published.

Related Posts