
WIKI YA HUDUMA NA GIRL GUIDES
Wiki moja kabla ya Maadhimisho ya Kumbukizi ya Waasisi wa Girl Guides duniani, Girl Guides hupaswa kushiriki katika Wiki ya Huduma (Service Week), ambapo kwa mwaka huu, Girl Guides kutoka mikoa 12 ya ki Girl Guides walipata nafasi ya kuandaa na kushiriki katika matukio mbalimbali ikiwemo, Kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa mahospitalini, kutembelea watoto yatima na wenye mahitaji maalum, lakini pia waliweza kushiriki katika kufanya usafi wa Mazingira uliohusisha moja kwa moja upandaji wa miti, na usafi wa maeneo ya shule na mazingira yanayowazunguka.